1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BRISBANE: Mshukiwa wa nane atiwa mbaroni

3 Julai 2007
https://p.dw.com/p/CBmM

Polisi nchini Australia wamemtia mbaroni mshukiwa wa nane kuhusina na njama za mashambulio ya mabomu mjini London Uingereza na shambulio la kigaidi kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa mjini Glasgow nchini Scotland.

Polisi walimkamata mwanamume wa umri wa miaka 27 aliyekuwa akijaribu kupanda ndege katika uwanja wa ndege wa Brisbane.

Mwanasheria mkuu wa Australia, Philip Rudock amewaambia waanidhishi wa habari mjini Canberra kuwa mshukiwa huyo alijaribu kuihama Australia akiwa hana tiketi ya kumuwezesha kurejea nchini humo.

Ruddock amesema mashtaka dhidi ya mwanamume huyo hayafunguliwa. Ruddock pia amesema mshukiwa huyo si raia wa Australia, lakini alikuwa akifanya kazi kama msajili katika hospitali ya Gold Coast ya jimbo la Queensland.

Mwanamume huyo sasa anawasaidia polisi katika uchunguzi.

Polisi wamefanya msako katika jimbo la Queensland usiku kucha na katika hospitali alikofanya kazi mshukiwa huyo lakini hakuna dalili zozote zinazoonyesha kuwa Australia inakabiliwa na hatari ya kushambuliwa.