1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Brown awasili China kwa zaira rasmi

18 Januari 2008
https://p.dw.com/p/CtM8

BEIJING:

Waziri Mkuu wa Uingereza-Gordon Brown- amewasili nchini China akiandamana na ujumbe mkubwa wa viongozi wa wafanya biashara. Hii ikiwa ndio ziara yake ya kwanza nchini humo kama waziri mkuu,kiini chake ni kuimarisha uhusiano wa kibiashara wa nchi hizo mbili.Pia Bw Brown atajadiliana na wakuu wa China, masuala mbalimbali yakiwemo ,suala la kubadilika kwa hali ya hewa,kukuza lugha ya Kiingereza pamoja na kuwawezesha wanawake wa China kujiimarisha katika nyanja zote.Miongoni mwa vigogo wa serikali ya China anaotarajiwa kukutana nao ni waziri mkuu Wen Jiabao pamoja na rais Hu Jintao.