1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BRUSSELS : Abbas ataka kuungwa mkono kwa serikali yake

24 Februari 2007
https://p.dw.com/p/CCP6

Rais Mahmoud Abbas wa Palestina amekuwa na mazungumzo na maafisa wa Umoja wa Ulaya mjini Brussels Ubelgiji katika jitihada za kutaka kuungwa mkono kwa serikali mpya ya umoja wa kitaifa ya Wapalestina.

Kiongozi huyo wa Wapalestina pia anataraji kuushawishi Umoja wa Ulaya kuanza tena kutowa msaada kwa Wapalestina ambao umesitishwa wakati kundi la Hamas lilipoingia madarakani zaidi ya mwaka mmoja uliopita.Katika mkutano na waandishi wa habari pamoja na mkuu wa masuala ya kigeni wa Umoja wa Ulaya Havier Solana Abbas amesema amekubali kwamba serikali mpya ya Palestina inayoundwa lazima itambuwe haki ya kuwepo kwa taifa la Israel na kukanusha matumizi ya nguvu.

Mapema hapo jana Rais Abbas alikutana na Kansela Angela Merkel wa Ujerumani mjini Berlin.