1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BRUSSELS: Eneo la Schengen kupanuliwa

9 Novemba 2007
https://p.dw.com/p/C78q

Mawaziri wa ndani wa Umoja wa Ulaya katika mkutano wao mjini Brussels wameidhinisha kuziingiza nchi 9 mpya katika kundi la nchi za Ulaya zisizohitaji ukaguzi wa pasipoti mipakani kuanzia mwezi wa Desemba.Hatua hiyo itarahisisha usafiri katika eneo la nchi hizo na kuchangamsha biashara na uchumi katika eneo linalojulikana kama eneo la Schengen.

Baada ya Desemba 20,vituo vya ukaguzi mpakani kwenye bandari na nchi kavu vitaondoshwa kati ya nchi 15 za Schengen za hivi sasa na hizo nchi 9 mpya ambazo ni Malta na nchi za Ulaya ya Mashariki.Waziri wa Ndani wa Ujerumani,Wolfgang Schauble amesema,hatua hiyo inatimiza ndoto ya kuwa na Ulaya moja baada ya kusambaratika kwa ukomunisti katika mwaka 1989.