1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BRUSSELS : Hakuna haja kuuwa magaidi kwa dhamira

13 Julai 2007
https://p.dw.com/p/CBjJ

Mkuu wa masuala ya sheria wa Umoja wa Ulaya amekataa pendekezo la waziri wa mambo ya ndani wa Ujerumani kwamba yumkini ikawa ni halali kuwauwa magaidi katika mauaji ya kuwalenga kwa makusudi

Kamishna wa Sheria wa Umoja wa Ulaya Franco Frattini ameviambia vyombo vya habari vya Ujerumani kwamba anapinga aina zote za adhabu ya kifo na kwamba kupambana na ugaidi hakuhitaji mauaji ya aina hiyo.

Waziri wa mambo ya ndani wa Ujerumani Wolfgang Schaeuble alitowa wazo hilo la kuuwa magaidi kwa kuwalenga kwa makusudi wakati wa mahojiano na gazeti la Ujerumani la Der Spiegel wiki hii.Schaueble anahesabiwa kuwa ni mtu wa siasa kali miongoni mwa wahafidhina wa chama cha Kansela Merkel cha Christian Demokratik.

Waziri huyo mara nyingi amekuwa akitowa mawazo ya hatua kali katika kupiga vita ugaidi.