1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Brussels: Kamisheni ya Ulaya inazisihi Russia na Belorussia zitanzuwe mzozo wao wa usafirishaji wa mafuta hadi Ulaya Magharibi.

9 Januari 2007
https://p.dw.com/p/CBHa

Tume ya Ulaya imezihimiza Russia na Belorussia ziutanzue kwa haraka mzozo wao juu ya bomba la mafuta ambao umepelekea Russia kusita kupeleka mafuta hadi sehemu fulani za Ulaya, kupitia Belorussia. Maafisa wa tume ya Ulaya wanasema Russia iko katika hatari ya kuonekana haiaminiki kutokana na mzozo huo wa nishati. Maafisa wa Belorussia wamewasili Mosko kufanya mazungumzo juu ya mzozo huo. Jana Russia ilisita kupeleka mafuta hadi nchi za Ulaya kupitia bomba linalopitia Druzhba, Belorussia, wakiwatuhumu Wa-Belorussia kwamba wanayachukuwa mafuta hayo kwa njia isiokuwa ya halali. Belorussia inashikilia kwamba Russia ilipe dola 45 kwa tani moja ya kubiki kwa mafuta yanayopitia kwenye bomba lililo katika ardhi yake, lakinI Russia inasema karo hiyo sio ya halali

Na Kansela Angela Merkel wa Ujerumani amesema kusita hivi sasa kuja mafuta kutoka Russia hadi Ulaya Magharibi kuimedhihirisha haja ya Ujerumani kuwa na njia nyingine za kupitia nishati inayoihitaji. Akizungumza katika televisheni ya Ujerumani, alisema serekali yake inahitaji kuzingatia matokeo ya mipango ya sasa ya kutaka kupunguza kutumia nishati ya kinyukliya:

+ Tokeo hili, bila ya shaka, halijaleta athari kubwa sana katika sisi kupata nishati, lakini katika miaka ya karibuni yametokea kila wakati matatizo juu ya ya mafuta hayo yanakopitia hadi kuja hapa Ujerumani. Tunataka uhakika wa kisheria, tunataka uhakika katika mikataba tuliotia saini, na jambo hilo sasa linaonesha lazima lipanuliwe kiziingiza nchi ambazo mafuta hayo yanapitia…+