1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BRUSSELS: Kundi jipya kujadili uhuru wa Kosovo

21 Julai 2007
https://p.dw.com/p/CBgc

Marekani na washirika wake katika Umoja wa Ulaya,wameamua kuachilia mbali mswada wa azimio linalopendekeza kutoa uhuru kwa jimbo la Kosovo. Uamuzi huo,umesifiwa na Serbia,lakini Wakosovo wamesema ni jambo la kusikitisha.Waziri Mkuu wa Serbia,Kojislav Kostunica amesema,Serbia ikiungwa mkono na mshirika wake Urusi,pamoja na kura ya turufu ya Urusi katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa,zimetetea umoja wa Serbia na jimbo lake la Kosovo,lenye wakazi wengi wenye asili ya Kialbania.Siku ya Ijumaa,Marekani na nchi za Umoja wa Ulaya,zilikubali kulikabidhi kundi la mataifa sita,jukumu la kushughulikia suala la Kosovo.