1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BRUSSELS: Mjerumani kuuwakilisha Umoja wa Ulaya

29 Julai 2007
https://p.dw.com/p/CBe2

Umoja wa Ulaya umemteua mwanadiplomasia wa Kijerumani,Wolfgang Ischinger kuwakilisha umoja huo wenye nchi 27,katika majadiliano yajayo kuhusu hatima ya jimbo la Kiserbia la Kosovo. Mkuu wa sera za kigeni wa Umoja wa Ulaya,Javier Solana amesema,Ischinger alie na miaka 61, ataungana na wajumbe wa Marekani na Urusi kujadiliana hatima ya Kosovo.

Serbia imeupinga mpango wa Umoja wa Mataifa unaopendekeza kutoa uhuru kwa jimbo la Kosovo, chini ya usimamizi wa kimataifa.

Ischinger ambae hivi sasa ni balozi wa Ujerumani nchini Uingereza,anajulikana kama ni mtaalamu wa eneo la Balkan.