1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BRUSSELS: Mkataba mpya wa Umoja wa Ulaya ni hatua kubwa

P.Martin28 Juni 2007

Kansela Angela Merkel wa Ujerumani amekamilisha kipindi chake cha miezi sita kama rais wa Umoja wa Ulaya kwa kuwahotubia wabunge wa umoja huo, mjini Brussels.

https://p.dw.com/p/CHC1
Kansela Angela Merkel akihotubia Bunge la Umoja wa Ulaya mjini Brussels
Kansela Angela Merkel akihotubia Bunge la Umoja wa Ulaya mjini BrusselsPicha: AP

Merkel aliwaambia wabunge hao, maafikiano ya mkataba mpya wa Umoja wa Ulaya yaliyopatikana juma lililopita,yameondosha vikwazo katika umoja huo ulio na wanachama 27.

Amesema mkataba huo ni hatua kubwa mbele na utarahisisha utaratibu wa kupitisha maamuzi na kuwaleta karibu zaidi wakazi wa Umoja wa Ulaya. Mkataba huo unachukua nafasi ya katiba iliyokataliwa.Siku ya Jumapili,Ujerumani itaikabidhi Ureno wadhifa wa urais wa Umoja wa Ulaya.