1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BRUSSELS: Mkutano wa kilele wa Umoja wa Ulaya wamalizika

9 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCKn

Mkutano wa kilele wa Umoja wa Ulaya uliozungumzia nishati umemalizika leo mjini Brussels, Ubelgiji. Viongozi wa umoja huo wamefikia makubaliano ya pamoja kuhusu matumizi ya nishati yanayolenga kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa. Makubaliano hayo yanaweka kiwango cha asilimia 20 cha matumizi ya nishati mbadala katika mataifa ya Umoja wa Ulaya kufikia mwaka wa 2020.

Makubaliano hayo yamefikiwa baada ya Ujerumani kufanya mabadiliko katika mapendekezo yanayoeleza vipi wanachama 27 wa umoja huo watakavyochangia kufikia viwango vya Umoja wa Ulaya.

Akizungumza baada ya mkutano wa mjini Brussles kumalizika, waziri mkuu wa Uhispania, Jose Manuel Barroso, amesema, ´Uhispania inaongoza barani Ulaya katika swala la nishati safi na tutaendelea kufanya utafiti na kuwekeza katika eneo hili. Pamoja na Ujerumani sisi ni taifa muhimu zaidi katika nishati inayotokana na upepo.´

Mkataba uliofikiwa unaeleza hatua tofauti za kwanza zinazotakiwa kuchukuliwa na mataifa wanachama kupunguza gesi inayotoka viwandani.

Hatua hiyo ilinuiwa kuzihimiza nchi kama Ufaransa inayotegemea sana nishati ya nyuklia na Poland inayotumia makaa ya mawe zisaini mkataba huo.