1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BRUSSELS: Moto misituni yaua watu 44

25 Agosti 2007
https://p.dw.com/p/CBVy

Umoja wa Ulaya utatoa msaada kwa Ugiriki kupambana na moto unaozidi kusambaa na kuteketeza vijiji na misitu.Ujerumani,Ufaransa na Norway zinapeleka helikopta na ndege za kuzima moto.Hadi hivi sasa,si chini ya watu 44 wamepoteza maisha yao katika moto huo,kusini mwa Ugiriki.Idadi kubwa ya wahanga ni kutoka kijiji cha Zaharo, magharibi ya Peleponnes.