1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BRUSSELS: Mwito kubadili mbinu za kupambana na Taliban

15 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CC1t

Ujerumani imetoa mwito wa kubadilisha mbinu zinazotumiwa na muungano wa vikosi vinavyoongozwa na Marekani kupambana na wanamgambo wa Kitaliban nchini Afghanistan.Mwito huo umetolewa baada ya kutokea kwa mfululizo wa maafa ya kiraia nchini Afghanistan.Waziri wa ulinzi wa Ujerumani,Franz Josef Jung aliuambia mkutano wa mawaziri wa ulinzi wa Umoja wa Ulaya mjini Brussels,maafa ya aina hiyo yakiendelea,kuna hatari kwamba raia wa Afghanistan watakuwa na chuki dhidi ya vikosi vya ushirikiano vinavyoongozwa na Marekani.Juma lililopita,vikosi hivyo vilithibitisha kuwa zaidi ya wakazi 40 wa vijijini waliuawa katika mashambulio ya angani yaliyolenga wanamgambo wa Taliban,kusini mwa Afghanistan.