1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BRUSSELS : Steinmeir athibitisha kupotea kwa Wajerumani 2

12 Februari 2007
https://p.dw.com/p/CCSq

Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Frank Walter Steinmeir amethibitisha mjini Brussels kwamba Wajerumani wawili wamekuwa hawajulikani walipo kwa wiki moja sasa lakini haijulikani iwapo wametekwa nyara.

Steinmeir alithibitisha hayo kabla ya kukutana na mawaziri wenzake wa mambo ya nje wa Umoja wa Ulaya wanaokutana mjini Brussels kwa mkutano wao wa kila mwezi.

Steinmeir pia amesema kwamba serikali inafanya kila iwezalo kuhakikisha kuachiliwa kwa Wajerumani hao na kurudi nyumbani salama.

Mwaka jana Wajerumani wawili Rene Bräunlich na Thomas Nitzschke walitekwa nchini Iraq na kuachiliwa bila ya kudhuriwa miezi mitatu baadae.

Miezi kadhaa kabla mtaalamu wa machimbo ya kale Susanne Osthof alishikiliwa mateka kwa wiki kadhaa.