1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BRUSSELS: Ujerumani iongoze juhudi za kupambana na ongezeko la joto

8 Aprili 2007
https://p.dw.com/p/CCBc

Kamishna wa mazingira wa Umoja wa Ulaya,Stavros Dimas ametoa wito kwa Ujerumani kuchukua hatua zaidi kupambana na mabadiliko ya hali ya hewa. Dimas alitamka hayo katika mahojiano yake na gazeti la Kijerumani “Die Welt”,siku moja baada ya Umoja wa Mataifa kutoa ripoti yake ya pili kuhusu hali ya hewa ikitabiri kuwa dunia inakabiliwa na maafa makubwa katika siku zijazo. Dimas amesema,malengo ya Umoja wa Ulaya kuhusu hali ya hewa,yataweza kutekelezwa kwa msaada wa Ujerumani tu,ikiwa ni nchi yenye uchumi mkubwa kabisa barani Ulaya.Ripoti ya Umoja wa Mataifa iliyotolewa siku ya Ijumaa mjini Brussels,imesema ongezeko la joto duniani litasababisha hasara kubwa katika mabara yote upesi kuliko ilivyotarajiwa hapo awali.Kwa mujibu wa ripoti hiyo,nchi zilizo masikini kabisa duniani ndio zitakazoathirika vibaya zaidi.