1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BRUSSELS : Ujerumani isiwekewe matumaini makubwa mno

14 Desemba 2006
https://p.dw.com/p/CCjU

Rais wa Tume ya Umoja wa Ulaya Jose Manuel Barroso ameonya kwamba mazungumzo na Uturuki kuhusiana na kujiunga kwa nchi hiyo na umoja huo yanaweza kuchukuwa miaka 15.

Viongozi wa Umoja wa Ulaya wanakutana mjini Brussels Ubelgiji leo hii suala la Uturuki likiwa juu kwenye agenda baada ya mawaziri wa mambo ya nje wa umoja huo kupendekeza kukawilishwa kwa mazungumzo ya Uturuki kujiunga na Umoja wa Ulaya hatua ambayo imeshutumiwa vikali na Uturuki kwamba haikuwa ya haki.

Na katika mahojiano na gazeti la kila wiki la Ujerumani Die Welt Rais huyo wa Tume ya Umoja wa Ulaya Jose Manuel Barrosso ametahadharisha dhidi ya kuwekewa matumaini makubwa mno kupindukia Ujerumani itakapochukuwa Urais wa Umoja wa Ulaya kuanzia mwezi wa Januari mwaka 2007.

Amesema wasitegemee matatizo yote ya Umoja wa Ulaya yatatuliwa na Ujerumani na kuongeza kusema kwamba wadhifa huo unadumu kwa miezi sita tu na sio miaka sita.