1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BRUSSELS : Ulaya kudhibiti kampuni za nishati za kigeni

30 Agosti 2007
https://p.dw.com/p/CBUM

Gazeti la Financial Times la Ujerumani limesema Halmashauri ya Umoja wa Ulaya inafikiria udhibiti katika kuzuwiya makampuni ya nishati ya kigeni hususan ya Urusi na Saudi Arabia kununuwa makampuni ya gesi na umeme ya Ulaya yalioko kwenye matatizo.

Imesema nchi wanachama wa Umoja wa Ulaya zina mashaka kwamba Umoja wa Ulaya ukiachilia ushindani zaidi katika mfumo wa makampuni makubwa ya nishati barani Ulaya kutapelekea makampuni madogo kuwa rahisi kununuliwa na makampuni yasio ya Umoja wa Ulaya yanayotaka kujishughulisha na usambazaji wa nishati.

Mojawapo ya makampuni hayo ni kampuni ya gasi ya taifa ya Urusi Gazprom.

Msemaji wa halmahsuri hiyo amekiri kwamba rasimu juu ya suala hilo inasambazwa kwa nchi wanachama lakini amekataa kuizungumzia.