1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BRUSSELS : Ulaya yataka Libya iwaachie huru wanamatibabu

29 Desemba 2006
https://p.dw.com/p/CCfR

Umoja wa Ulaya hapo jana umeisihi Libya kuwaachilia huru wauguzi wa Kibulgaria na daktari mmoja wa Kipalestina wanaotuhumiwa kuwaambukiza virusi vya HIV watoto wa Libya baada ya mahkama ya Libya kuamuwa kuithibitisha tena hukumu yao ya adhabu ya kifo.

Katika baruwa kwa Wizara ya mambo ya nje ya Libya Mkuu wa Masuala ya Nje wa Umoja wa Ulaya Benita Ferrero –Waldner amesema kwamba ni matumaini yake makubwa kuwa maafisa husika wa serikali ya Libya watachukuwa hatua zinazohitajika kutowa nafasi ya kufikiwa na mapema kwa ufumbuzi wa kesi hiyo kwa msingi wa kibinaadamu.

Watu hao sita wamekuwa gerezani tokea mwaka 1999 kwa madai kwamba wamewambukiza kwa makusudi virusi vya HIV zaidi ya watoto 400 katika hospitali moja ya mji wa Benghazi wakati wa kufanya jaribio lililokwenda kombo la kutafuta tiba ya UKIMWI.

Watoto 50 kati ya hao walioambukizwa virusi vya HIV tayari wamekufa.