1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BRUSSELS :Ulaya yatowa azimio lao juu ya Iran

25 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CCzU

Mataifa ya Ulaya yamesambaza rasimu ya azimio lake yenyewe lenye kutaka kuwekewa vikwazo kwa Iran baada ya kushindwa kufikia makubaliano na serikali ya Marekani.

Maafisa wa Marekani wamesema wana imani mzozo huo utatatuliwa lakini haijulikani lini.Msimamo wa pamoja kati ya Marekani na Uingereza,Ufaransa na Ujerumani ambazo zilikuwa wasuluhishi wakuu katika mazungumzo na Iran ni muhimu kwa juhudi za kimataifa kukomesha mpango wa nuklea wa Iran ambao mataifa ya magharibi yanasema unakusudia kutengeneza silaha za nuklea wakati Iran ikisema ni kwa ajili ya kuzalisha nishati.

Hata hivyo washirika hao inaonekana kutafautiana juu ya baadhi ya masuala ikiwa ni pamoja na dai la Marekani kutaka Urusi ilazimishwe kusitisha shughuli zake katika mtambo wa Bushehr wa kuzalisha umeme kwa nguvu za nuklea nchini Iran.