1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BRUSSELS : Umoja wa Ulaya kuikaripia Uturuki

8 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCuv

Tume ya Umoja wa Ulaya baadae leo hii inatazamiwa kutowa repoti yenye kushutumu maendeleo yaliofikiwa na Uturuki katika harakati zake za kuwania uwanachama wa Umoja wa Ulaya.

Kitengo hicho kikuu cha utendaji cha Umoja wa Ulaya hakitegemewi kupendekeza kusitishwa kwa mazungumzo ya Uturuki kujiunga na umoja huo.

Repoti hiyo itaonyesha kwamba kasi ya mageuzi nchini Uturuki imepiga hatua kubwa lakini kwa hivi karibuni kasi hiyo imeanza kuzorota. Hususan masuala ya kuendelea kwa vitendo vya utesaji na kushindwa kwa Uturuki kuruhusu uhuru wa kutowa maoni yanatazamiwa kutiliwa mkazo.

Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani wa Frank Walter Steinmeir amekuwa akijaribu kutuliza mzozo huo.

Repoti hiyo pia itataja kugoma kwa Uturuki kufunguwa bandari zake kwa meli za Cyprus.

Cyprus ni nchi mwanachama wa Umoja wa Ulaya na mikataba iliopita na serikali ya Uturuki na Umoja wa Ulaya inataja kwamba meli kutoka nchi zote wanachama wa Umoja wa Ulaya zinaruhusiwa kuingia kwenye bandari za Uturuki.