1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BRUSSELS: Umoja wa Ulaya kuisaidia Peru

17 Agosti 2007
https://p.dw.com/p/CBYH

Halmashauri ya Umoja wa Ulaya imeahidi kutoa kiasi cha euro milioni moja kwa ajili ya misaada ya dharura kwa waathirika wa tetemeko la ardhi lililotokea juzi Jumatano nchini Peru.

Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari inasema uamuzi huo umepitishwa na idara ya misaada ya kibinadamu ya halmashauri hiyo, ECHO, kuzisaidia juhudi za mashirika yasiyo ya kiserikali na mashirika ya misaada ya Umoja wa Mataifa katika eneo hilo lililokumbwa na mtetemeko huo wa ardhi.

Juhudi hizo zitajumulisha ujenzi wa makaazi, utoaji wa huduma za matibabu na chakula.

Hali halisi katika eneo lililoathiriwa na tetemeko la ardhi kwa sasa haijulikani kwa sababu ya ukosefu wa njia za kwenda katika eneo hilo.

Watu takriban 500 waliuwawa na wengine zaidi ya 1,000 kujeruhiwa katika tetemeko hilo.