1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BRUSSELS : Umoja wa Ulaya wapongeza uchaguzi wa Congo

31 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CCxZ

Umoja wa Ulaya umepongeza marudio ya uchaguzi wa rais katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo hapo jana kwa kiasi kikubwa kufanyika kwa amani.

Mkuu wa misaada wa Umoja wa Ulaya Lois Michel amesema Wacongomani milioni 25 waliokuwa na uwezo wa kupiga kura wameweka historia kwa kukamilisha uchaguzi huo kufuatia miongo kadhaa ya machafuko.Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Kofi Annan pia ameupongeza uchaguzi huo kwa kufanyika katika mazingira ya uhuru na utulivu licha ya kuwa na wasi wasi juu ya matukio ya matumizi ya nguvu katika jimbo la Equateur na karibu na Bunia katika wilaya ya Ituri.

Wagombewa wote wawili Rais anayetetea wadhifa huo Joseph Kabila na mpinzani wake Jean Piere Bemba mfanya bishara na kiongozi wa zamani wa waasi wamewataka wananchi wa Congo kuepuka matumizi ya nguvu.

Umoja wa Ulaya una wanajeshi wa kulinda amani 2,000 nchini Congo wakiwemo wanajeshi 800 wa Ujerumani.

Kuna jumla ya wanajeshi wa kulinda amani 17,000 wa Umoja wa Mataifa nchini humo.