1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BRUSSELS: Umoja wa Ulaya wazisihi Korea ya kaskazini na Iran kurejea kwenye mazungumzo juu ya mpango wa kinyuklia

18 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CD1o

Umoja wa Ulaya umezisihi nchi za Korea ya kaskazini na Iran kusikia mwito wa jumuiya ya kimataifa na kurejea kwenye meza ya mazungumzo juu ya mpango wa kinyuklia. Waziri wa mambo ya kigeni wa Ujerumani, Frank-Walter Steinmeir, alisema mawaziri wa mambo ya kigeni wa nchi wanachama wa Umoja wa Ulaya hawana chaguo jingine isipokuwa tu kushinikiza vikwazo vya kuiadhibu Korea ya kaskazini kufuatia kitendo chake cha kuripua bomu la kinyuklia tarehe 9 mwezi huu.

Nchi wanachama wa Umoja wa Ulaya ziliunga mkono vikwazo vya Baraza la usalama la Umoja wa mataifa lakini kila moja kwa upande wake. Ujerumani imekwenda mbali zaidi kuanza mbinyu kiasi dhidi ya Iran bila hata hivyo kufunga milango ya mazungumzo.