1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BRUSSELS : Umoja wa Ulaya yajadili Kosovo

12 Februari 2007
https://p.dw.com/p/CCSt

Mjumbe wa Umoja wa Mataifa Marti Ahtisaari leo hii amewataarifu mawaziri wa mambo ya nje wa Umoja wa Ulaya juu ya pendekezo lake juu ya hadhi ya baadae la jimbo la Kosovo ikiwa ni siku moja baada ya Walabania wawili kufariki kutokana na ghasia dhidi ya mpango huo wa Umoja wa Mataifa.

Waziri wa mambo ya nje wa Austria Ursula Plassnik amesema machafuko hayo sio kitu kizuri hususan katika hali ya mvutano. Amesema anataraji hilo litakuwa kumbusho kwa kila mtu jinsi ilivyo muhimu kuleta utulivu.

Serikali mjini Belgrade imekataa rasimu ya mpango huo wa Ahtisaari kwa kusema kwamba italigawa taifa la Serbia kwa kuipa uhuru jimbo hilo la kusini lenye wakaazi milioni mbili asilimia 90 wakiwa ni kabila la Waalbania.

Mawaziri wa mambo ya nje wa Umoja wa Ulaya katika mkutano huo wa Brussels wanatazamiwa kuunga mkono mpango huo wa Ahtisaari.