1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Brussels. Uturuki yatoa pendekezo kufungua viwanja vyake vya ndege na bandari kwa Cyprus.

8 Desemba 2006
https://p.dw.com/p/CClT

Mabalozi wa umoja wa Ulaya wanatarajiwa kukutana baadaye leo kwa ajili ya kikao maalum kujadili pendekezo la Uturuki la kufungua bandari na viwanja vyake vya ndege kwa ajili ya vyombo vya usafiri vya Cyprus. Inafikiriwa kuwa wanaweza kuamua kuwaambia mamawaziri wa mambo ya kigeni wa umoja wa Ulaya kutochukua hatua ya kusitisha kwa muda mazungumzo na Uturuki.

Hata hivyo kwa mujibu wa wanadiplomasia wa umoja wa Ulaya pendekezo hilo la Uturuki lina masharti kwa serikali ya Wagiriki wa Cyprus kuweza kukubaliana na mambo fulani. Serikali ya Uturuki haitambui serikali hiyo ya Wagiriki wa Cyprus. Umoja wa Ulaya unataka Uturuki kufungua bandari zake zote pamoja na viwanja vya ndege kwa ajili ya vyombo vya usafiri vya Cyprus.