1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BRUSSELS: Wito wa kukaza vikwazo dhidi ya Sudan

6 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCLy

Umoja wa Ulaya umetoa wito kwa Umoja wa Mataifa kufikiria kukaza vikwazo dhidi ya Sudan kuhusika na jimbo la mgogoro la Darfur.Serikali ya Khartoum imekataa kuviruhusu vikosi vya amani vya Umoja wa Mataifa kuungana na wanajeshi 7,000 wa Umoja wa Afrika katika jimbo hilo magharibi ya Sudan.Mawaziri wa masuala ya nje wa Umoja wa Ulaya wanaokutana mjini Brussels,wamesema wana wasiwasi mkubwa kuhusu hali ya usalama inayozidi kuwa mbaya huko Darfur na wamewalaumu waasi na pia wanamgambo wanaoungwa mkono na serikali ya Sudan.Vile vile wamelaani mashambulio yanayofanywa dhidi ya miradi ya kiutu na wafanyakazi wa mashirika yanayotoa misaada ya kiutu.Juma lililopita,Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu nchini Uholanzi ilisema inataka kufungua mashtaka dhidi ya waziri mmoja wa Sudan na kiongozi wa wanamgambo wa Janjaweed wanaoiunga mkono serikali.Mashtaka hayo yanahusika na uhalifu dhidi ya utu.