1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BRUSSELS:EU kupeleka jeshi Darfur

24 Julai 2007
https://p.dw.com/p/CBfv

Mawaziri wa Nje wa Umoja wa Ulaya wamekubaliana kuanza mipango ya uwezekano wa kupeleka kikosi cha askari elfu 3000 wa kulinda nchini Chad.

Kikosi hicho cha Umoja wa Ulaya kinategemewa kulinda usalama wa maelfu ya wakimbizi kutoka Darfur waliyokimbia Sudan toka mwaka 2003.

Hata hivyo Umoja huo wa Ulaya umesisitiza kuwa ni lazima jeshi hilo lipate baraka za Umoja wa Mataifa na kwamba litafanyakazi kwa kushirikiana na jeshi la kulinda amani la Umoja wa Afrika na Umoja wa Mataifa lililoko huko kusini mwa Sudan.

Ufaransa huenda ikatoa mchango mkubwa katika kikosi hicho, ambacho kinatarajiwa kuanza kazi yake katika kipindi cha miezi sita ijayo.

Mzozo wa miaka minne wa Darfur umesababisha vifo vya watu zaidi ya laki mbili na wengine zaidi ya milioni mbili kutokuwa na makazi.