1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BRUSSELS:NATO yalalamika juu ya hatua ya Urusi kujitoa kwenye mkataba

15 Julai 2007
https://p.dw.com/p/CBif

Nchi za mfungamano wa kijeshi wa NATO zimeeleza wasi wasi juu ya hatua ya Urusi kusimamisha utekelezaji wa mkataba juu ya kudhibiti silaha za kawaida barani Ulaya.

Rais Vladimir Putin wa Urusi ametia saini agizo juu ya hatua hiyo itakayoanza kutekelezwa na Urusi baada ya siku 150 kwa mujibu wa mkataba huo.

Hatahivyo naibu waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani bwana Gernot Erler amesema bado pana muda wa kuuokoa mkataba huo.Bwana Erler ameeleza kuwa mlango wa kufikia mapatano bado haujafungwa kabisa.