1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BRUSSELS:Umoja wa Ulaya wapinga adhabu ya kifo Texas

22 Agosti 2007
https://p.dw.com/p/CBWz

Umoja wa Ulaya umepaaza sauti kupinga adhabu ya kifo ya mia nne inayotarajiwa kutekelezwa katika jimbo la Texas nchini Marekani.Rais wa sasa wa tume ya Umoja huo, Ureno katika tamko, imemtaka Gavana wa jimbo la Texas atumie mamlaka yote aliyokuwa nayo ili azuie utekelezaji wa adhabu hiyo.

Adhabu hiyo ya kifo inatarajiwa kutolewa kwa Ray Conner kwa kosa la mauaji.

Ikiwa itatekelezwa ,mtu huyo atakuwa wa mia minne kunyongwa katika jimbo la Texas tokea kurudishwa tena adhabu ya kifo katika jimbo hilo mnamo mwaka 1976.