1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BRUSSELS:Uturuki yakubali kufungua bandari zake kwa Cyprus

7 Desemba 2006
https://p.dw.com/p/CClo

Nchi ya Uturuki imekubali kufungua bandari yake moja vilevile kiwanja cha ndege ili kuruhusu ndege na meli za Cyprus kupita.Hii inatokea kufuataia hatua ya Umoja wa Ulaya kusimamisha kwa muda mazungumzo ya Uturuki kujiunga na umoja huo kwasababu ya kuikataza Cyprus kutumia bandari zake kwa biashara na usafiri.

Hata hivyo Uturuki kupitia msemaji wake Mikko Norros bado haijafafanua bandari zitakazofunguliwa au lini.Umoja wa Ulaya umekuwa ukitisha kusimamisha mazungumzo yaliyoanza mwaka mmoja uliopita ya kuirihusu Uturuki kuwa mwanachama.Wiki jana Tume ya Ulaya ilipendekeza kusimamishwa kwa muda mazungumzo hayo kwa kuwekea vikwazo vipengee inavyohitajika kutimiza kabla kuwa mwanachama.

Suala hilo limesababisha mitizamo tofauti katika Umoja wa Ulaya ulio na mataifa 25 wanachama wanaojaribu kufikia makubaliano fulani watakapokutana mjini Brussels,Ublegiji jumatatu ijayo.

Mazungumzo hayo ya kuirihusu Uturuki kujiunga na Umoja wa Ulaya huenda yakadumu kwa miaka kumi bila kuwa na hakikisho lolote kwamba itakubaliwa kujiunga.