1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BRUSSELS:Viongozi wa EU wajadilia muafaka wa katika

21 Juni 2007
https://p.dw.com/p/CBpe

Viongozi wa Umoja wa Ulaya wanakutana mjini Brussels nchini Ubelgiji ili kuafikiana kuhusu katiba mpya ya Jumuiya hiyo.

Kansela wa Ujerumani Bi Angela Merkel aliye pia mwenyekiti wa Umoja wa Ulaya anatoa wito kwa viongozi wenzake kushirikiana ili kufikia muafaka.

Kamishna wa Umoja wa Ulaya Jose Manuel Barroso aliyehudhuria kikao hicho anasisitiza umuhimu wa kufanya mabadiliko ili jumuiya hiyo iweze kukimu mahitaji ya nchi wanachama.Umoja wa Ulaya una nchi 27 wanachama.

Nchi za Poland na Uingereza zinaonya kutumia kura ya turufu endapo pingamizi zao hazitashughulikiwa ipasavyo.Poland inashtumu mfumo wa upigaji kura uliopendekezwa na Ujerumani kwa kueleza kuwa mataifa madogo wanachama hayatapata nafasi.Uingereza kwa upande wake inatoa wito wa kupata hakikisho kuwa sheria na uhuru wake hautaathirika vilevile sera zake za kigeni.Makubaliano hayo mapya yanalenga kuondoa katiba ya zamani iliyopingwa na kuangushwa katika kura za maoni nchini Ufaransa na Uholanzi.