1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BRUSSELS:Wafanyibiashara wa Ulaya walalamikia mfumko wa bidhaa rahisi kutoka China na Vietnam

4 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CD6E

Umoja wa Ulaya umekubaliana kutoza ushuru wa ziada viatu vya bei rahisi vinavyoingizwa kutoka China na Vietnam katika mataifa ya Ulaya.

Hatua hii imechukuliwa na Umoja huo ili kuzuia mfumko wa uingizwaji bidhaa za bei rahisi kutoka nchi hizo mbili.

Ushuru huo wa ziada utatozwa katika kipindi cha miaka miwili badala ya miaka mitano kama ilivyotaka tume ya Ulaya.

Nchini Ujerumani kiasi ya asilimia 60 ya viatu vinavyouzwa vinatokea China na Vietnam.Wafanyibiashara nchini humu wanasema uingizwaji wa bidhaa hizo za bei rahisi unaharibu ushindani wa kibiashara.