1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BRUSSLES: Bunge la Ulaya lajadili ripoti ya uchunguzi kuhusu shirika la CIA

14 Februari 2007
https://p.dw.com/p/CCSG

Bunge la Ulaya linajadili ripoti ya uchunguzi wa mwaka mmoja kuhusu madai kwamba shirika la ujasui la Marekani, CIA, liliwazuilia kisiri washukiwa wa ugaidi barani Ulaya na kuwasafirisha kwa ndege katika mataifa yanayofanya vitendo vya mateso. Ripoti hiyo inatarajiw kupigiwa kura hii leo kwenye bunge hilo la Ulaya.

Ripoti hiyo inazilaumu serikali zaidi ya 10 za mataifa wanachama wa Umoja wa Ulaya yakiwemo Ujerumani, Uingereza, Poland na Hispania kwa aidha kujua kuhusu safari za siri za washukiwa wa ugaidi au kutumika kama vituo vya safari za ndege za shirika la ujasusi la CIA. Ripoti hiyo hata hivyo haitoi ushahidi.

Wabunge wengi wanasema madai katika ripoti hiyo yatatakiwa yapunguzwe ili yaweze kuungwa mkono na vyama vingi bungeni.