1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BUCHAREST: Ujerumani yatwaa urais wa Umoja wa Ulaya.

1 Januari 2007
https://p.dw.com/p/CCeE

Ujerumani imetwaa urais wa Umoja wa Ulaya ambao una wanachama wawili wapya, Bulgaria na Romania.

Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Frank Walter-Steinmeier alihudhuria sherehe za kukabidhiwa wadhifa huo zilizofanyiwa Bucharest ambapo alizungumzia hali hiyo kama mwisho wa mgawanyiko wa kihistoria wa bara la Ulaya.

Steinmeier anatarajiwa baadaye leo kutembelea mji mkuu wa Bulgaria, Sofia.

Wakati huo huo Slovenia imeidhinisha matumizi ya sarafu ya Yuro na hivyo kuwa taifa la kwanza lililokuwa likifuata siasa ya ukomunisti kuanza kutumia sarafu hiyo.