1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BUDAPEST: Maandamano mapya kumpinga Gyurcsany

8 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CD4q

Nchini Hungary,kiasi ya watu 15,000 wameandamana mbele ya bunge,mjini Budapest wakimtaka waziri mkuu Ferenc Gyurscany aondoke madarakani. Maandamano hayo mapya ya kumtaka ajiuzulu, yanafanywa baada ya Gyurscany kufanikiwa kuungwa mkono katika kura ya imani iliyopigwa bungeni siku ya Ijumaa.Wimbi la kwanza la maandamano lilianaza mwezi wa Septemba,baada ya kufichuliwa kwa ukanda wa sauti.Katika tepu hiyo waziri mkuu anasema kuwa alisema uwongo kuhusu hali ya uchumi ili kupata kuchaguliwa tena katika uchaguzi uliofanywa mwezi wa April.