1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Budapest. Waandamanaji wataka waziri mkuu ajiuzulu.

7 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CD5M

Mamia kwa maelfu ya waandamanaji wameandamana nje ya bunge la Hungary mjini Budapest wakidai kujiuzulu kwa waziri mkuu wa nchi hiyo Ferenc Chuksanyi.

Maandamano hayo yamekuja baada ya waziri mkuu huyo kunusurika katika kura ya kutokuwa na imani nae kuhusiana na kukiri kwake kuwa alidanganya kwa wapiga kura ili kuweza kupata ushindi mwezi wa Aprili.

Jana Ijumaa , Chuksanyi aliomba radhi bungeni kwa kudanganya na kushindwa kutatua matatizo ya kiuchumi ya Hungary.