1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BUENOS AIRES: Mwanamke kuongoza nchini Argentina

29 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/C7BT

Argentina,kwa mara ya kwanza imemchagua mwanamke kushika wadhifa wa juu serikalini.Baada ya kuhesabiwa kwa zaidi ya asilimia 80 ya kura,Bibi Cristina Fernandez de Kirchner alie na umri wa miaka 54 amejisombea asilimia 44 ya kura zilizopigwa katika uchaguzi wa siku ya Jumapili. Yeye ni mke wa rais anaeondoka madarakani,Nestor Kirchner.