1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BUENOS AIRES: Rais wa kwanza wa kike nchini Argentina

29 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/C7BZ

Mke wa Rais Kirchner wa Argentina anaeondoka madarakani,ametangazwa mshindi wa uchaguzi wa rais uliofanywa siku ya Jumapili.Baada ya kuhesabiwa takriban asilimia 75 ya kura zilizopigwa,Bibi Cristina Fernandez de Kirchner anaongoza kwa kujinyakulia kiasi ya asilimia 44 ya kura.Bibi Kirchner alie na miaka 54 anatazamiwa kuwa rais wa kwanza wa kike nchini Argentina.