1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BUENOS AIRES: Rais wa zamani kukamatwa

12 Januari 2007
https://p.dw.com/p/CCbT

Mahakama moja nchini Argentina imeamuru rais wa zamani wa nchi hiyo, Isabel Peron, atiwe mbaroni kwa kupotea kwa mwanaharakati wa mrengo wa kushoto katika miaka ya 1970.

Kiongozi huyo wa zamani anatafutwa pia kwa kusainiwa kwa sheria zinazomhusisha na makundi ya mauaji. Watetezi wa haki za binadamu wanasema makundi hayo yaliwaua wapinzani takriban 1,500 wa serikali kati ya mwaka wa 1973 na 1976.

Isabel Peron alichukua madaraka kufuatia kifo cha mumewe, Juan Domingo Peron, aliyeitawala Argentina kwa awamu tatu.

Jaji wa mahakama kuu ametoa waranti wa kukamatwa kwa Isabel kupitia shirika la polisi la kimataifa, Interpol, katika juhudi ya kumkamata Peron nchini Hispania ambako anaishi hivi sasa.