1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BUENOS AIRES: Uchaguzi wa rais wafanyika leo

28 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/C7CB

Raia wa Argentina wanapiga kura hii leo kumchagua rais wao mpya huku mke wa rais wa nchi hiyo akitarajiwa kushinda.

Cristina Fernandez de Kirchner, ana nafasi kubwa ya kuchaguliwa kuwa rais wa kwanza mwanamke wa Argentina.

Rais anayeondoka madarakani, Nestor Kirchner, anang´atuka baada ya kuitawala Argentina kwa awamu moja ya miaka minne.