1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Buenos Aires.Agentina yaifungulia mashtaka Iran.

26 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CCzF

Waendesha mashtaka nchini Argentina wameifungulia mashtaka Iran na wanamgambo wa Kishia wa kundi la Hezbollah, kufuatia shambulio la bomu la mwaka 1994 dhidi ya kituo cha jumuiya ya wayahudi mjini Boenos Aires.

Waendesha mashtaka nchini Argentina wametoa waranti wa kimataifa dhidi ya Rais wa zamani wa Iran Akbar Hashemi Rafsanjani na maafisa wengine sita.

Israel na Marekani kwa muda mrefu wamekuwa wakiilaumu Iran kwa kuhusika kupanga na wanamgambo wa Hezbollah ili kufanyika kwa shambulio hilo, tuhuma ambazo Iran imezikanusha.

Shambulio hilo lilipelekea kuuwawa kwa watu 85 na wengine 300 kujeruhiwa.