1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Bujumbura. Katibu mkuu wa zamani akamatwa.

27 Aprili 2007
https://p.dw.com/p/CC6T

Aliyekuwa katibu mkuu wa chama cha CNDD FDD nchini Burundi , Bwana Hussein Rajabu amekamatwa na polisi leo alasiri.

Hii inakuja baada ya bunge la nchi hiyo kumvua kinga ya ubunge mwanasiasa huyo baada ya ombi la mwendesha mashtaka mkuu wa serikali kutaka Rajabu aondolewe kinga hiyo.

Kwa muda wa siku mbili Rajabu amekuwa akifika mbele ya mahakama baada ya kutuhumiwa na polisi nchini humo kwamba alikuwa na nia ya kupanga uasi.

Hussein Rajabu ni mmoja kati ya waasisi wa chama cha waasi wa zamani cha CNDD FDD ambacho hivi sasa kiko madarakani.