1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BUJUMBURA : Serikali yapinga kuachiliwa watuhumiwa

7 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CD5T

Mahakama Kuu ya Burundi hapo jana iliwaachilia kwa muda mahabusu saba wanaoshukiwa kuhusika katika njama ya mapinduzi lakini waendesha mashtaka haraka walikata rufaa dhidi ya hukumu hiyo na kuwaamuru maafisa wa magereza kutotii uamuzi huo wa mahkama.

Polisi ilimkamata rais wa zamani wa nchi hiyo Domitien Nadayizeye na watu wengine sita hapo mwezi wa Augusti kwa kusema kuwa walikuwa na ushahidi mzito kwamba walikuwa wakipanga njama ya kumuuwa Rais Pierre Nkuruzinza na kuipinduwa serikali.

Lakini watuhumiwa hao wamesema madai hayo yamebuniwa ili kuzima upinzani na imetaka mahkama iwaachilie uhuru wakati kesi hiyo ikiendelea kusubiriwa.Katika hukumu yake hapo jana Mahkama Kuu imesema ombi la kuongeza muda wa kuwashikilia watuhumiwa gerezani halikubaliki.

Mwendesha mashtaka mkuu wa serikali nchini Burundi Jean Bosco Ndikumana amekataa rufaa ya haraka na kumuamuru mkuu wa gereza kuu la Bujumbura kutowaachilia watuhumiwa hao.