1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BUJUMBURA.Kundi la mwisho la waasi lajiunga na serikali

19 Februari 2007
https://p.dw.com/p/CCQj

Kundi la mwisho la waasi nchini Burundi limejiunga na serikali katika kamati linayoshughulikia utekelezaji wa hatua muhimu ya kusimamishwa mapigano chini ya upatanishi wa bwana Charles Nqakula wa Afrika Kusini.

Hatua hiyo inamaliza mgomo wa kundi hilo wa miezi kadhaa.

Viongozi wakuu wa kundi la National Liberation Force FNL leo walijiunga pamoja katika kamati inayoshughulikia kutekelezwa makubaliano yaliyotiwa saini mwezi septemba mwaka uliopita kati ya serikali ya Burundi na kundi hilo la FNL.

Kundi hilo la FNL ndilo la pekee kati ya makundi ya waasi lililobaki nje ya makubaliano ya amani ya mwaka 2002.