1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Bundesliga yanukia kwa Hannover na Stuttgart

15 Mei 2017

Klabu ya Hannover iliwabwaga vinara wa ligi ya daraja la pili nchini Ujerumani Stuttgart 1-0 Jumapili, na sasa timu hizo zimefungana kipointi kileleni mwa jedwali la ligi hiyo.

https://p.dw.com/p/2d0D6
Fußball 2. Bundesliga Hannover 96 - VfB Stuttgart
Mchezaji wa Hannover Miiko Albornoz akipambana na Christian Gentner wa Stuttgart katika mechi ya JumapiliPicha: picture-alliance/dpa/P. Steffen

Hili lina maana ya kwamba timu hizo zinakaribia kujikatia nafasi ya kurejea katika ligi kuu ya Bundesliga msimu ujao.

Felix Klaus alicheka na wavu katika dakika ya 40 ya mechi na kuchelewesha kupandishwa daraja kwa Stuttgart, huku kukiwa kumesalia mechi moja kwa kila timu msimu kufikia kikomo.

Eintracht Braunschweig ambayo ndiyo timu ya pekee inayoweza kuwafikia Hannover na Stuttgart kimahesabu, iko alama tatu nyuma yao baada ya kucharazwa 6-0 na Arminia Bielefield, ikiwa ina magoli 6 nyuma ya Hannover na Stuttgart ikiwa imewashinda na mabao 10.

Hannover na Stuttgart zote zilishushwa daraja kutoka ligi kuu ya Bundesliga msimu uliopita. Braunschweig wao kwa sasa wamejihakikishia kwamba watamaliza katika nafasi ambayo watawezwa kupandishwa daraja au kucheza mechi ya mchujo na timu itakayomaliza ya tatu kutoka chini katika msimamo wa Bundesliga, ambapo kulingana na mambo yalivyo sasa ni Hamburg.

Mwandishi:Jacob Safari/ap

Mhariri:Josephat Charo