1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Bundesliga yasimama wapi Ulaya ?

Ramadhan Ali13 Novemba 2007

Ligi ya Ujerumani-Bundesliga iko hadhi gani miongoni mwa klabu mashuhuri za Ulaya ? Kwanini timu za Ujerumani kitambo sasa haziwiki katika vikombe vya Ulaya ? ilikuwa 2001 mara ya mwisho kwa klabu ya Ujerumani-munich kuvaa taji.

https://p.dw.com/p/CHar
Stadi wa W.Bremen katika B-Liga.
Stadi wa W.Bremen katika B-Liga.Picha: AP

Bundesliga-Ligi ya Ujerumani ni kali kiasi gani miongoni mwa Ligi mashuhuri ulimwenguni ?

Swali hili limeibuka baada ya timu za Ujerumani kushindwa kutamba msimu huu katika champions League-kombe la klabu bingwa barani ulaya .

Sifa za kabumbu la Ujerumani zimeanza kutiliwa shaka nah ii ni mwaka tu tangu Ujerumani kumaliza nafasi ya tatu nyuma ya Itali na Ufaransa katika kombe la dunia na timu yake ya wasichana imeibuka majuzi mabingwa wa dunia.

Tuma Dandi anasimulia:

Kwa muujibu wa mwnyekiti wa klabu ya bayern Munich,mchezaji wa zamani wa timu ya Taifa Karl-Heinz-Rummenigge,klabu za Ujerumani zinaonewa na hazina tena fursa sawa katika daraja ya juu ya dimba la Ulaya .Hii anadai Rummenigge yatokana na kutogawanywa sawa inavyostahiki kwa mapato ya fedha katika dimba la Ulaya.

Kwahivyo asema Rummenigge,

“hakuna meneja au kocha duniani awezae kufidia upungufu huo wa usawa katika mashindano ya dimba.”

Bayern munich, klabu ya Bw.Rummenigge na mwenzake Beckenbauer,ni mojawapo ya timu 6 za Bundesliga iliopigwa kumbo wiki iliopita nje ya vikombe vya Ulaya.Klabu za Ujerumani kwa kweli, zimecheza vibaya mno kuliko wakati wowote mnamo miaka 52 iliopita ya kinyan’ganyiro cha vikombe vya Ulaya.

Baada ya kushindwa mara 4 mfululizo, mabingwa wa Bundesliga VFB Stuttgart hawamo tena katika kinyan’ganyiro cha champions League wakati Werder Bremen na Schalke zinapigana kufa-kupona kubakia mashindanoni.

Katika kombe la Ulaya la UEFA ,Bayern Munich viongozi wa Ligi wakati huu walizimwa sare tena nyumbani na Bolton Wanderers ya Uingereza wakati Nüremberg,majirani zao huko kusini walilazwa nyumbani na Everton.Bayer Leverkusen ikatimuliwa nje na Spartak Moscow.

Ukosefu dhahiri wa wezani wa nguvu sawa kifedha una maana kwamba Bundesliga-Ligi ya Ujerumani yanunua wingi wa wachezaji lakini sio mastadi –adai Rummenigge.

Mnamo misimu mingi ,Bundesliga imekuwa ikiteremka chini ya daraja ya miaka 5 iliowekwa na UEFA-shirikisho la dimba la Ulaya.

Mara ya mwisho kwa timu ya Bundesliga kucheza finali ya kombe la Ulaya ilikua 2002 na kati ya timu 20 za Ulaya zilizofika finali tangu enzi hizo,Spian imetwaa mataji mara 5,Itali na Uingereza mara 4 kila moja ,ureno mara 3 ,Ufaransa mara 2 na Scotland na Russia kila moja mara 1.

Kwa jicho hilo,asemayo Karl-Heinz Rummenigge ,ni sawa yana uzito.Ujerumani kwa kitita chake cha Euro milioni 420 inayovuna kutoka mapato ya TV,kila mwaka, iko nyuma sana na Ligi ya Uingereza inayovuna Euro bilioni 1.1,Itali Euro milioni 735,Ufaransa Euro milioni 618 na Spian Euro milioni 575.

Sura hii haitii lakini maanani kuwa Ujerumani inavuna fedha nyingi zaidi kuliko Ligi nyengine kupitia matangazo ya biashara ,uhisani na mauzo ya zana za kispoti kwa mashabiki.Isitoshe, Ujerumani inajivunia idadi kubwa ya mashabiki wendao viwanjani ulimwengu ni.Ujerumani na Itali ziko nyuma tu ya mapato ya Uingereza.

Kisingizio cha upungufu wa fedha ndio chanzo cha kutotamba kwa dimba la Ujerumani barani Ulaya sio hoja inayokubaliwa na wengi katika dimba la Ujerumani.

Rais wa shirikisho la dimba la Ujerumani (DFB) Theo Zwanziger,anasema mengi zaidi yahitaji kufanywa kuboresha utoaji wa mafunzo ya kabumbu na kuwaendeleza chipukizi.

Katika msimamo wake huo, anaungwamkono na kocha wa Taifa wa Ujerumani Joachim Loew.Katika mazungumzo na jarida la dimba-KICKER-, ameungama kwamba dimba la Ujerumani linahitaji kuendelezwa upande fulani.Lothar Matthaeues ,alieicheza Ujerumani mara nyingi kabisa anasema pia, hoja ya fedha nyingi katika Ligi nyengine haina uzito katika kuelezea msiba wa dimba la klabu za Ujerumani.

“siwezi tena kusikia hayo zaidi.Tunachokosa ni hamasa,jazba na ari ya kucheza dimba.Na hizo ndizo sifa timu kutoka Ufaransa,Ugiriki ambako hakuna fedha nyingi zinatuonesha.”

Bayern munich mabiongwa mara 4 wa Ulaya miaka ya nyuma walitwaa kombe la klabu bingwa barani Ulaya mara ya mwisho 2001.Munich ingali inahesabika mojawapo ya timu bora kabisa za Ulaya licha ya kutoshiriki msimu huu katika champions League na kuponea kucheza kombe la UEFA.

Munich ilibadili sera zake msimu huu ilipotumia kitita cha Euro milioni 70 kununua wachezaji stadi kabisa kama mfaransa Franck Ribery, mtaliana Luca Toni na mjerumani Miroslav Klose na hivyo Munich ni miongoni mwa timu zinazopigiwa upatu kutwaa kombe la UEFA msimu huu.

Timu ya taifa ya Ujerumani, halkadhalika, imekata bila ya taabu tiketi yake ya kucheza finali za kombe la ulaya la mataifa hapo mwakani-Euro 2008- na itateremka uwanjani huko Uswisi na Austria, kama mojawapo ya timu bora kabisa zinazopigiwa upatu kutwaa kombe.