1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Bunge Cyprus, kupigia kura ya uokozi

Admin.WagnerD18 Machi 2013

Wakati bunge la nchini Cyprus leo hii linajiandaa kupiga kura mapendekezo ya fedha za uokozi kutoka katika kanda inayotumia sarafu ya euro, Urusi imesema mapendekezo hayo ni hatari na yasiyo ya haki kwa taifa hilo.

https://p.dw.com/p/17zSM
epa03629604 A Cypriot press and information office handout photograph shows Cypriot President Nicos Anastasiades speaking the people of Cyprus in a televised address , Nicosia, Cyprus late 17 March 2013, following the 16 March bailout agreement reached at a Eurogroup meeting to rescue the banking sector and the island`s economy. The President said the agreement may be painful but it was the only option EPA/CYPRIOT PRESS OFFICE / HANDOUT EDITORIAL USE ONLY/NO SALES EDITORIAL USE ONLY/NO SALES +++(c) dpa - Bildfunk+++
Rais Nikos Anastasiades wa CyprusPicha: picture-alliance/dpa

Hatua hiyo inayotarajiwa sasa itafikiwa baada ya mjadala mrefu ulioahirishwa mara kadhaa kwa lengo la kufanikisha mashauriano kuhusu suala hilo tata.

Wiki iliyopita katika mkutano wake uliyofanyika Brussels, kanda inayotumia sarafu ya euro ilikadiria  kiasi cha euro bilioni 10 ikiwa sawa na dola za kimarekani bilioni 13 kwa lengo la kukikwamua kiuchumi kisiwa hicho kilichopo katika bahari ya Mediterranean.

Makato yanayolaumiwa

Wanaoweka fedha  zao katika mabenki watakabiliwa na makato fulani ya kodi. Kwa mfano mwenye kiasi cha  mpaka euro 100,000 watatozwa kiasi cha asilimia 6.75 na zaidi ya akiba hiyo kiwango cha tozo kinaweza kufikia mpaka asilimia 9.9.

People queue to use an ATM machine outside of a Laiki Bank branch in Larnaca, Cyprus, Saturday, March 16, 2013. Many rushed to cooperative banks which are open Saturdays in Cyprus after learning that the terms of a bailout deal that the cash-strapped country hammered out with international lenders includes a one-time levy on bank deposits. The move, decided in an extraordinary meeting of the finance ministers of the 17-nation eurozone in the early hours Saturday, is a major departure from established policies. Analysts have warned that making depositors take a hit threatens to undermine investors' confidence in other weaker eurozone economies and might possibly lead to bank runs. (AP Photo/Petros Karadjias)
Raia wa wakitoa pesa katika mashine za kutolea fedhaPicha: picture-alliance/AP

Mpango huo wa fedha za uokozi ulikuwa upigiwe kura jana, lakini baadae alasiri ukaahirishwa mpaka leo hii. Rais Nicos Anastasiades wa Cyprus ameonya pasipo fedha hizo sekta ya kifedha ya taifa hilo itaporomoka, na kulitupungiza taifa katika mkwamo wa kiuchumi kwa kufirisika kabisa.

Matumaini finyu ya kupitisha mkopo

Kiongozi huyo anaungwa mkono na viti 28 kati ya viti 56 vya bunge la taifa hilo ambalo kwa uamuzi wake unatorajaiwa unaelezwa, unaweza kuliondoa taifa hilo katika mkwamo.

Portugal's Finance Minister Vitor Gaspar (L), European Commissioner for Economic and Monetary Affairs Olli Rehn and Cyprus Finance Minister Michalis Sarris attend a euro group finance ministers meeting at the European Union Council in Brussels March 15, 2013. REUTERS/Eric Vidal (BELGIUM - Tags: POLITICS BUSINESS)
Viongozi wanaoiwakilisha kanda inayotumia sarafu ya euroPicha: Reuters

Hata hivyo vyama viwili vya upinzani AKEL na EDEK vimemekwisha sema haviungi mkono mpango huo wa uokozi kutoka kanda inayotumia safari ya euro.

Katika hatua nyingine iliyochukuliwa mwishoni mwa juma mabenki yamezuia akanuti za wafunga akaunti za wateja wao ile ya kawaida pamoja na ya njia ya mtandao kwa lengo la kuzuia wateja wenye hasira kuchukua fedha zao katika mabenki kutokana na kukasirishwa na mapendekezo hayo.

Urusi yalalamikia mpango wa kanda ya euro

Kwa kawaida jumatatu ni siku ya mapunziko kwa shughuli za kibenki, benki zote zinafungwa nchini Cyprus lakini kwa mujibu wa vyombo vya habari nchini humo serikali itaendelea kuzifunga taasisi zake za fedha hata kesho kwa lengo la kudhibiti kuendelea kwa shughuli za kibenk.

Russian President Vladimir Putin speaks during a news conference in Moscow, Russia, Thursday, Dec. 20, 2012. Putin says a draft bill banning U.S. adoptions of Russian children is a legitimate response to a new U.S. law that calls for sanctions on Russians deemed to be human rights violators. But he has not committed to signing it. (Foto:Misha Japaridze/AP/dapd)
Rais wa Urusi Wladimir PutinPicha: dapd

Wakati ukisubiria uamuzi wa bunge la Cyprus katika kuamua hatima ya mpango huo wa fedha za uokozi Rais wa Urusi Vladimir Putin amekosoa vikali kwa kusema si wa haki na hakuna mfano wa hatua kama hiyo iliyowahi kutokea.

Kupitia msemaji wa Ikulu ya Kremlin, Dmitry Peskov, rais Putin amesisitiza kwamba mpango huo utakuwa wa hatari, usio wa haki na sio wa kitaalamu.

Idadi kubwa ya raia wa Urusi, wameweka kiasi kikubwa cha mabilioni ya euro mabenki ya Cyprus kwa utaratibu wa akaunti za kigeni, na mabenki ya urusi yamewekeza pia katika taifa hilo kibiashara.

Mwandishi: Sudi Mnette/RTR/AFP
Mhariri: Mohammed Khelef