1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Bunge la Ujerumani kurefusha muda wa shughuli za wanajeshi wa ujerumani Afghanistan

12 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/C7GS

Berlin:

Bunge la shirikisho Bundestag limeanza mjadala kuhusu kurefushwa muda wa shughuli za jeshi la Ujerumani Bundeswehr nchini Afghanistan.Wabunge wanatazamiwa kuupigia kura mchana huu mswaada wa serikali kuu kama shughuli hizo zirefushwe kwa mwaka mmoja au la.Kwa maoni ya mkuu wa kundi la wabunge wa chama cha SPD bungeni Peter Struck, shughuli za jeshi la Ujerumani zinaweza kudumu miaka kumi nchini Afghanistan.