1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ulaya kupigia kura marekebisho ya sheria za waomba hifadhi

Tatu Karema
10 Aprili 2024

Wabunge wa Umoja wa Ulaya watapiga kura ya kuzifanyia marekebisho makubwa sera za utoaji hifadhi za umoja huo ambazo zitaimarisha taratibu za mipakani kwa waomba hifadhi wanaowasili katika maeneo hayo kinyume cha sheria

https://p.dw.com/p/4ec14
Bunge la Ulaya
Bunge la Ulaya kupigia kura marekebisho ya sheria za waomba hifadhiPicha: Jean-Francois Badias/AP/picture alliance

Makubaliano hayo mapya ya Uhamiaji na Ukimbizi yanajumuisha sheria 10 zilizoundwa baada ya miaka mingi ya mazungumzo ambayo yanalenga kuzifanya nchi za Ulaya, zote zikiwa na vipaumbele tofauti vya kitaifa, kuchukua hatua za pamoja katika suala la uhamiaji, kwa kutumia sheria sawa.  

Ikiwa sheria hata moja itakosa kupitishwa, makubaliano hayo hayatafikiwa.

Makundi makuu ya kisiasa ya bunge hilo la Ulaya yameashiria kuunga mkono mkataba huo. Vyama vya mrengo mkali wa kulia na kushoto vinapinga baadhi ya sheria hizo.

Mashirika ya misaada na yasiyo ya kiserikali pia yamejitokeza kupinga makubaliano hayo, ambayo yanayaona kama nia ya kufanya kuwa vigumu zaidi kwa wakimbizi kutafuta hifadhi na ulinzi.