1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Bunge laidhinisha sheria ya kuwajumuisha wanachama wa Baath katika serikali.

13 Januari 2008
https://p.dw.com/p/Cou9

Baghdad.

Bunge la Iraq limeidhinisha sheria ambayo inatoa nguvu ya kurejeshwa kwa waungaji mkono wa chama cha Baath nchini humo kushika nyadhifa katika serikali. Maafisa wa Marekani wamesema kuwa hatua hiyo ni muhimu kuelekea maridhiano ya kitaifa. Kura ilipigwa bungeni kwa kunyoosha mkono katika kila kifungu cha sheria hiyo yenye vifungu 30. Sheria hiyo ya uwajibikaji na sheria kama inavyofahamika rasmi, inataka kulegeza vikwazo kwa haki ya wanachama wa zamani wa chama cha Saddam Hussein kuweza kushika nyadhifa katika serikali.