1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Buriani Birgit Prinz

12 Agosti 2011

Mfungaji katika timu ya taifa ya wanawake Ujerumani, Birgit Prinz amestaafu. Je mchango na ufanisi wake ni upi?

https://p.dw.com/p/12Fp9
Birgit Prinz anasema ni uamuzi alio utafakari vilivyoPicha: picture alliance/dpa

Birgit Prinz ambaye ni mshindi mara mbili wa mashindano ya kombe la dunia, mwenye umri wa miaka 33, amelitangaza hilo mwezi mmoja baada ya kustaafu kutoka timu ya taifa baada ya timu hiyo kutolewa kwenye robo fainali za mashindano ya kombe la dunia mwaka huu na timu ya Japan.

Frauenfußball-WM 2011 Deutschland Birgit Prinz Ersatzbank
Prinz hapa katika mashindano yaliomalizika ya kombe la dunia, katika kundi A, Ujerumani ilipocheza dhidi ya NigeriaPicha: dapd

Mchango na mafanikio yake:

-Ameshiriki mechi 214 kati ya mwaka 1994 hadi 2011.


-Amefunga mabao 128.


-Alishinda kombe la dunia 2003 na 2007 na la ubingwa wa Ulaya mara tano.


-Alichaguliwa mchezaji bora mwanamke 2003 na 2005.


-Ni mshindi wa nishani ya shaba mara tatu katika mashindano ya olimpiki.

Nafasi ya wachezaji wa zamani Ujerumani

Kwengineko, kulikuwa na wakati ambapo kuwa mchezaji wa zamani wa kimataifa nchini Ujerumani kulitoa hakikisho la kupata ajira, lakini hili siku hizi limebadilika. Wachezaji wengi wa zamani wa timu ya taifa ya Ujerumani, sasa wanalazimika kutafuta timu kucheza kandanda.

Wachezaji wa kulipwa wanakabiliwa na wakati mgumu kwa kuwa wengi wao wanataka mishahara mikubwa. Na katika matumaini ya kupata kandarasi, wachezaji wengi wapo tayari kufanya mazoezi na timu za divisheni ya pili na kupata kusafiri sehemu tofauti.

Wachezaji kama David Odonkor mwenye umri wa miaka 27 na Gerald Asamoah mwenye umri wa miaka 32, wanajifunza kwenye timu ya divisheni ya tano huku kipa, Timo Hildebrand, mwenye umri wa miaka 32, alisafiri hadi nchini Marekani kupata kushiriki katika mechi ya mazoezi na timu ya Uingereza Manchester United lakini alikuwa hakusajiliwa.

EURO 2008 David Odonkor Deutschland Tenero Training
David OdonkorPicha: picture alliance/dpa

Andreas Hinkel mwenye umri wa miaka 29, na aliyekuwa akizichezea timu ya Stuttgart na Glasgow Celtic katika kiungo cha ulinzi, yupo katika umri ambapo angekuwa sasa ndiyo anatamba kwenye mchezo huo, lakini anajipata katika hali walizomo wachezaji wengine wa zamani wa Ujerumani.

Hivi sasa anajifunza tu na Stuttgart licha ya kuwa mkurugenzi wa timu hiyo hawezi kumhakikishia kusajiliwa.

Ligi ya Ujerumani Bundesliga ikiwa inaongozwa na mabingwa watetezi msimu huu, Borussia Dortmund, zimewajumuisha wachezaji chipukizi kwenye timu.

Jambo linalosababisha ushindani kuwa mkubwa kwa kuwa wachezaji wameendelea na wengi ni wenye umri wa miaka 19, zaidi ya ilivyokuwa siku za nyuma.

Wachezaji chipukizi ambao wengi huwa tayari kucheza kwa kiwango kilicho chini kidogo.

Ulf Baranovsky wa muungano wa wachezaji kandanda Ujerumani, anasema kuwa angependekeza wachezaji hao wa zamani wafikirie kucheza katika timu za kiwango cha chini na pia kwa kiwango hicho kidogo cha malipo. Na kuwa iwapo watafanya hivyo watakuwa na nafasi nzuri za kupata kandarasi.

Bundesliga mwishoni mwa juma

Na katika orodha ya ushindani wa timu mwishoni mwa juma hili katika ligi hiyo ya Ujerumani, ambapo baadaye hii leo Borussia Moenchengladbach inateremeka dimbani dhidi ya Stuttgart, na hapo kesho Kaiserslautern inaonana na FC Augsburg.

Fußball Bundesliga Borussia Moenchengladbach gegen SC Freiburg
Picha: dapd

Huku nayo Bayer Leverkusen baada ya kufanikiwa kumsajili kipa chipukizi kwa mkopo kutoka Stuttgart, Bernd Leno, baada ya kipa wake Fabian Giefer kuumia kichwa katika pambano dhidi ya Mainz na kumsababisha apoteze ufahamu wa yaliotokea katika mwezi mmoja uliopita.

Leverkusen iliyofungwa mabao 2-0 kwenye mechi hiyo, hapo kesho itakabiliana na Werder Bremen.

Mwandishi: Maryam Abdalla/Dpae/Rtre
Mhariri:Josephat Charo